Habari zenu wadau wote wa App ya mapenzi!!
Leo napenda nitoe elimu au nishauri mambo mawili matatu kuhusu suala zima la mahusiano au mapenzi kwa rika zote ambazo zina vigezo vya kuingia kwenye mahusiano,namaanisha VIJANA na WATU WAZIMA.
Hivyo kabla sijaanza kutoa elimu ya mambo mbalimbali kuhusu MAHUSIANO/MAPENZI,lazima tujue nini maana ya hivyo vitu viwili na tofauti zake.Tukianza na MAHUSIANO.MAHUSIANO ni hali wanayokuwa nayo watu wawili au kikundi cha watu wakiwa wanashare vitu fulani,kwa mfano kuna mahusiano ya ndugu,hawa wanashare UDUGU,lakini pia kuna mahusiano ya marafiki,hawa wanashare URAFIKI,na mwisho kuna mahusiano ya wapenzi,hawa wanashare MAPENZI.Hizo zote ni maana na tofauti za mahusiano,tuje tuangalie na upande mwingine wa MAPENZI ni nini maana yake?! MAPENZI ni matakwa ya watu wawili (wakike na wakiume) kuamua kuwa kwenye mahusiano ya KIMAPENZI.Hii ni imekuwa mada kubwa sana siku hizi duniani,mada hii imekuwa ikiongelewa sana,kutungiwa nyimbo mbalimbali zikielezea faida nyingine hasara na changamoto mbalimbali zinatokana na mada hii ya MAPENZI.
Mapenzi huwa mazuri pale tu unapopata wa "type" yako kwani raha ya MAPENZI ni kupata UMPENDAYE nae AKUPENDE,sasa tatizo siku hizi mtu unampata unaempenda lakini yeye moyo wake upo kwa mtu mwingine,jambo hili limechangia sana mafumanizi hadi mauaji na hatimaye kuacha watoto wakiwa yatima pamoja na watoto wa mitaani,nini cha kufanya kupunguza au kuondoa kabisa changamoto kama hizi?!
JIBU:
1.Kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya mapenzi,chunguza kwanza mtu unayekwenda kuanza nae mahusiano kama kweli yupo serious na wewe na ana mapenzi ya kweli,usimpende mtu kwa sababu ya kitu au prsa alizokuwa nazo,kumbuka kila kitu tumekikuta duniani hapa.
2.Baada ya kuchunguza na kupata uhakika wa mtu unaempenda na yeye anakupenda,sasa kuna maisha baada ya ndoa ni ndani ya nyumba maisha halisi ya wanandoa tuanze na 6 kwa 6.Kama mumeo hakuridhishi sio sababu ya kuanza kutoka nje ila kuna njia nyingi za kufanya na mkatatua matatizo yenu bila hata kupelekana kwa wazazi au kuchepuka (KWA WANAWAKE).Ni njia zipi ninazomaanisha hapa?! Namaanisha mnatakiwa mkae mjadili cha kufanya ili kuilinda ndoa yenu,mfano;-Kumshauri mumeo afanye mazoezi,Pika vyakula husika vinavyohitajika kuboresha n.k lakini sio kutoka nje ya ndoa au kumuanika mumeo kwa majirani na ndugu.
Kwa leo nitaishia hapa,nitarudi na mada nyingine kuhusu mahusiano.
PASCHAL
gidebzo@gmail.com